Connect with us

Michezo

Yanga yateua Kamati ya Mashindano


By MWANDISHI WETU

KAMATI ya Utendaji  ya klabu ya Yanga imeunda kamati mpya ya mashindano itakayokuwa chini ya Mwenyekiti, Rodgers Gumbo.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na klabu hiyo kwenda kwenye vyombo vya habari, imesema  Kamati ya  Utendaji ya Yanga chini ya Mwenyekiti  Mshindo Msolla imeunda kamati hiyo mpya ya mashindano yenye wajumbe 13
Wajumbe wanaounda kamti hiyo ni Injinia Hersi Said, Beda Tindwa,Thobias Lingalangala, Edward Urio, Max Komba, Salum Mkemi, Yossuphed Mhandeni, Yanga Makaga, Adonis Bitegeko, Injinia Heriel Mhulo, Isaack Usaka, Injinia Deo Muta na Hassan Hussein.
Hiyo inakuwa kamati ya tisa ndani ya klabu hiyo huku ikiwa ya tano kuundwa tangu Mwenyekiti Msolla aingie madarakani Mei 5 mwaka huu.
Kamati nyingine  za klabu hiyo ni  Kamati ya Usajili, Kamati ya Sheria na Nidhamu, Kamati ya Hamasa na Uchangiaji, Kamati ya Matawi ya Wanachama, Kamati ya Kudumu ya Hamasa, Kamati ya   Ufundi na Kamati ya Ujenzi.


Source link

Comments

More in Michezo