Azizi Ki hatimaye asajiliwa tena Yanga – Julai 10

HATIMAYE Imejulikana, Mashabiki wa Wapenzi wa Yanga waliokuwa roho juu, presha inapanda na kushuka sasa hali shwarii. Ni baada ya uongozi wa klabu hiyo kufanya jitahida za kumbakiza klabuni hapo Kiungo wao Stephen Aziz Ki.

Taarifa iliyotoka muda mfupi kutoka Yanga inaeleza kwamba mchezaji huyo ataendelea kusalia klabuni hapo, na hivyo zile habari zote zilizokuwa zinasambaa kuwa anaondoka ni rasmi zimekufa tena.

Awali kulikuwa na tetesi za Aziz Ki kuhitajika na vilabu vikubwa Afrika kama vile Kaizer Chiefs, Mamelod Sundwons, na CR Belouizdad lakini baada ya kauli ya Injinia Hersi ni kama alikoleza moto wa utammbulisho w Aziz Ki.

Na baada ya kuwasili nchini mapema alfajiri ya leo, Aziz Ki aliongea na mashabiki wa Yanga kisha akawambia “Habari Wananchi bado niko hapa (Yanga)”

Mapema kabla ya haabri hizi Soka la Bongo tulisema kwamba Aziz Ki ataendelea kusalia Yanga kutoka na kauli tatu (3) kutoka kwa Rais wa klabu hiyo Injia Hersi Said, yeye mwenyewe mchezaji na kocha wake Miguel Gamondi.

KAULI YA KWANZA ILIYOKAA KIMKAKATI.

“Ni mkakati wa klabu kuhakikisha mchezaji anabaki na majadiliano yanaendelea vizuri na hapana shaka tutarudi kufanya utambulisho ingawa kuna klabu nyingi zinamhitaji mchezaji.”

“Hivyo majadiliano yanaendelea na ninaweza kusema kuna nafasi kubwa kwa mchezaji kubakia lakini hatujakamilisha.

“Aliweka wazi kuwa anataka kubaki unajua nilimsaini miaka miwili iliyopita na nilimsajili kutoka Asec Mimosas na nikamueleza kuhusu ‘project’ yangu na nani nataka waipeleke klabu katika ngazi za juu na akawa sehemu muhimu ya program na mpango, ambao upo hi vyo majadiliano yakawa yaleyale na alisema wazi kuwa nahitaji kubaki hapa na kuipeleka Yanga katika ngazi ambazo unataka ifike.

“Lakini mpira ni biashara sasa unaweza kusema unataka kubaki lakini hali ya kifedha ikabadilisha mawazo kwa hiyo naweza kusema ni 60/40 (uwezekano wa kubaki),” alisema Hersi.

KAULI YA  PILI YA AZIZ KI MWENYEWE.

“Dube anakuja, (Joseph) Guede yupo, nisikilize, mimi ni kiungo, nitafanya kila liwezekanalo kuhakikisha wanakuwa wafungaji bora. Mimi ni kiungo kwa nini niwanie ufungaji bora, kwa nini ununue straika halafu utake kiungo awe mfungaji bora.

“Mimi ahadi yangu, nina matumaini straika wa Yanga atakuwa mfungaji bora msimu ujao Mungu akipenda, lakini sio Aziz, sahau kuhusu Aziz, mimi nitatoa asisti na siyo kuwa mfungaji bora,” alinukuliwa Aziz Ki katika moja ya mazungumzo yake.

KAULI YA GAMONDI.

Kocha wa Yanga, Miguel Gamondi alisisitiza kuwa anahitaji kumkuta kiungo huyo kambini pindi atakapojiunga nayo na sio vinginevyo.

Kumekuwa na hisia kwamba uongozi wa Yanga umeshamalizana na mchezaji huyo na unachokifanya kwa sasa kutangaza kuwa hajasaini mkataba mpya ni kujaribu kutengeneza thamani ya tukio la utambulisho wa mkataba mpya wa mchezaji huyo.

Hisia hizo zinaweza kuthibitishwa na mmoja wa wajumbe katika uongozi wa Yanga ambaye hakupenda jina lake kutajwa ambaye alifichua kuwa Aziz Ki atakuwa kwenye kambi ya timu hiyo Afrika Kusini.

“Kambi ya maandalizi ya msimu mpya tutafanya Afrika Kusini na Aziz Ki atajiunga na timu huko hatuna wasiwasi wowote,” alisema kiongozi huyo.

Exit mobile version