Connect with us

Michezo

Usajili wa pesa nyingi wa Mourinho


LONDON, ENGLAND . JOSE Mourinho anafahamika kama moja ya makocha bora kabisa kuwahi kutokea kwenye mchezo wa soka na hakika kwenye kazi yake huyo amepata fursa ya kuwanoa mastaa wengi wenye viwango vya dunia.

Kwenye hilo la kufanya kazi na masta wengi, kuna wale ambao aliwapata kwa kulipa pesa nyingi sana.

Hii hapa ndio orodha ya wachezaji watano ambao Mourinho aliwanasa kwa pesa nyingi kwenye kipindi chake cha ukocha.

5. Andriy Shevchenko (AC Milan kwenda Chelsea) – Euro 43.8milioni

Chelsea walivunja tekodi yao ya uhamisho mwaka 2006 wakati walipomnasa Andriy Shevchenko kutoka AC Milan wakiamini kwamba wamenasa huduma matata. Lakini, mambo hayakuwa mazuri baada ya staa huyo kutua Stamford Bridge, ambapo aliishia kufunga mabao 23 tu kwa muda wake wa awamu mbili alizokuwa hapo kwani, alikwenda kwa mkopo pia Milan. Aliporudi alicheza mechi moja tu kisha akaondoka kwenda zake Dynamo Kyiv.

Advertisement

4. Nemanja Matic (Chelsea kwenda Man United)- Euro 44.7milioni

Kipenzi cha Jose Mourinho, Nemanja Matic alikuwa panga pangua kwenye kikosi cha Chelsea na kwamba lilitarajiwa lingekuwa jina la kwanza kusajiliwa baada ya kutua zake Manchester United. Hakika alifanya hivyo, Mourinho alinansa huduma ya kiungo huyo wa Kiserbia baada ya kutua huko Old Trafford. Alibaki kuwa mtumishi wake muhimu hadi hapo alipofutwa kazi na kuja Ole Gunnar Solskjaer, ambapo kwa sasa anamtia tu benchi kiungo huyo.

3. Fred (Shakhtar Donetsk kwenda Man United) – Euro 59milioni

Manchester United na Manchester City zilikuwa kwenye vita kali ya kusaka saini ya Fred kutokana na Mbrazili huyo kile alichokiwa akikifanya kwenye kikosi cha Shakhtar. Man United iliyokuwa chini ya Mourinho ilishinda vita hiyo na kunasa saini ya Fred kwenda kukipiga huko Old Trafford.

Lakini, Fred huyu wa Man United anaonekana kuwa tofauti kabisa na yule wa Shakhtar kutokana na kiwango chake cha uwanjani, amekuwa kawaida sana.

2. Romelu Lukaku (Everton kwenda Man United) – Euro 84.7milioni

Jose Mourinho siku zote amekuwa akimhusudu sana straika Romelu Lukaku baada ya kumsajili wakati akiwa Chelsea na baadaye alikuja kumsajili akiwa Manchester United mwaka 2017. Kwenye kipindi chake cha pili alizomsajili Mbelgiji huyo alimtoa Everton na hakika alilipa pesa nyingi kupata huduma yake, Euro 84.7 milionni. Alioondoka Old Trafford, maisha ya Lukaku yalibadilika chini ya kocha mpya na hivyo kuamua kuachana nan timu hiyo akitimkia zake Inter Milan.

1. Paul Pogba (Juventus kwenda Man United) – Euro 105milioni

Paul Pogba alirudi Manchester United kuliwa-shangaza wengi kutokana na pesa iliyolipwa kunasa sainni yake. Staa huyo kwa sasa ndiye mchezaji ghali zaidi kwenye kikosi cha Man United na ndiye mchezaji aliyenaswa kwa pesa nyingi na kocha Mourinho wakati alipowalipa Juventus, Euro 105 milionni kupata saini yake mwaka 2016.

Pogba bado yupo kwenye kikosi cha Man United, lakini mpango wake mkubwa kwa sasa ni kuachana na timu hiyo huku Real Madrid wakione-kana kuwa ndiko anakoe-lekea kwenda.






Source link

Comments

More in Michezo