Connect with us

Michezo

Uganda yamaliza Cecafa Wanawake kiroho safi


By Doris Maliyaga

KIKOSI cha timu ya soka ya Taifa ya Wanawake ya Uganda, licha ya kupata ushindi wa tatu kwenye michuano ya Chalenji Wanawake iliyofikia kikomo jana Jumatatu, wamechekelea.
Uganda iliyoanza mashindano hayo kwa kasi na lengo lao lilikuwa ni kuchukua ubingwa lakini Kenya iliyowachapa mabao 3-0, kwenye mechi ya nusu fainali, iliwaharibia kila kitu.
Ilicheza mshindi wa tatu na kuwafunga Burundi mabao 2-0, na kuwaacha Kenya ‘Harambee Starlets’ wakichukua ubingwa na nafasi ya pili ikienda kwa Tanzania Bara.
Kocha wa Uganda, Faridah Belega alisema: “Malengo yetu yalikuwa ni kutwaa ubingwa wa mashindano hayo lakini mambo hayakwenda sawa tukapata ushindi wa tatu.”
“Kwetu si mbaya, tunafurahi kwa sababu tumeondoka na kitu, lakini imetupa nafasi ya sisi kujiandaa zaidi kwa ajili ya mashindano mengine yajayo,”alisema Faridah.
Akizungumzia kiwango cha wachezaji wake, Faridah alisema amefurahishwa, isipokuwa matokeo ya mchezo mmoja tu wa Kenya.
“Upande wa kiwango wachezaji wamecheza kwa kiwango cha juu najivunia hilo, naamini siku zinavyozidi kusonga ndivyo timu itakuwa sawa zaidi. Tumeshinda mechi nne tumepoteza mmoja wa Kenya ni hatua,”aliongeza.
Uganda imechukua ushindi huo wa tatu katika mashindano hayo ambayo yalishirikisha jumla ya timu za mataifa manane kutoka Afrika Mashariki na Kati.
Timu zilizoshiriki ni pamoja na wenyeji Tanzania Bara, Uganda, Kenya Burundi, Djibouti, Sudan Kusini, Zanzibar na Ethiopia.


Source link

Comments

More in Michezo