Connect with us

Michezo

Tetesi za Soka Ulaya Jumapili 01.12.2019: Pochettino, Sanchez Flores, Rodgers, Howe, Silva, Arteta, Aubameyang, Depay

Pochettino ameshauriwa kutokimbilia kazi ya usimamizi katika klabu ya Arsenal na marafiki zake ambao wanaamini anaweza kupata kazi nzuri zaidiHaki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Pochettino ameshauriwa kutokimbilia kazi ya usimamizi katika klabu ya Arsenal na marafiki zake ambao wanaamini anaweza kupata kazi nzuri zaidi

Mkufunzi wa zamani wa Tottenham Mauricio Pochettino, ambaye amehusishwa na tetesi za kujiunga na Manchester United na Arsenal, atalazimika kulipa faini ya £12.5m akikubali kuajiriwa katika ligi ya Premia msimu huu. (Sunday Express)

Pochettino ameshauriwa kutokimbilia kazi ya usimamizi katika klabu ya Arsenal na marafiki zake ambao wanaamini anaweza kupata kazi nzuri zaidi. (Sunday Telegraph)

Watford imeitisha mkutano siku ya Jumapili ambao unadaiwa ajenda yake itakuwa kumfuta kazi Quique Sanchez Flores kwa mara ya pili. (The Athletic – subscription required)

Arsenal huenda ikasubiri hadi msimu ujao kumsajili mkufunzi Brendan Rodgers, lakini kocha huyo wa Leicester anachukulia nafasi ya Gunners kama kazi ya ndoto yake. (Star on Sunday)

Haki miliki ya picha
BBC Sport

Image caption

Arsenal huenda ikasubiri hadi msimu ujao kumsajili mkufunzi wa Leicester, Brendan Rodgers

Naibu mkufunzi wa Manchester City, Mikel Arteta ni mtu ambaye Arsenal inamtaka kuchukua nafasi ya Unai Emery. (Sunday Mirror)

West Ham inamfuatilia mkufunzi wamuda wa Arsenal, Freddie Ljungberg kama mrithi anayepigiwa upatu kuchukua nafasi ya Manuel Pellegrini. (Star on Sunday)

Jose Mourinho alipewa ofa ya £12m na Real Madrid kutochukua kazi nyingine ya ukufunzi ili asubiri Zinedine Zidane afutwe kazi kabla ya kujiunga na Tottenham. (Sun on Sunday)

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Kabla ya kujiunga na Tottenham, Jose Mourinho alipewa ofa ya £12m na Real Madrid kutochukua kazi nyingine ya ukufunzi ili asubiri Zinedine Zidane afutwe kazi

Everton inamtaka kocha wa Bournemouth, Eddie Howe, ambaye ni shabiki wa zamani wa klabu hiyo zama za ujana wake, kumrithi meneja Marco Silva anayekabiliwa na wakati hatari ya kufutwa katika klabu hiyo. (Sunday Mirror)

Real Madrid inapanga kuweka dau la £70m kumnunua mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30, huku kiungo wa kati wa Colombia James Rodriguez, 28, iikijumuishwa katika mpango huo. (Eldesmarque, via Star)

Chelsea inamfuatilia kwa karibu mchezaji Zaha na winga wa Borussia Dortmund na England Jadon Sancho, 19, inapojiandaa kuimarisha safy yake ya mashambulilizi. (Sunday Express)

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Real Madrid inapanga kuweka dau la £70m kumnunua mshambuliaji wa Arsenal na Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30,

Mshambuliaji wa Uhispania wa miaka 31-Diego Costa, ambaye alijiunga na Atletico Madrid kutoka Chelsea mwaka 2018, anatarajiwa kujiunhga na Flamengo kwa mkataba wa £25m. (Mundo Deportivo – in Spanish)

Liverpool na Tottenham wako tayari kumenyana katika kinyang’anyiro cha usajili wa mchezaji wa safu ya kati ya Lyon na Holland, Memphis Depay, 25. (Sunday Express)

Paris St-Germain bado haijampatia mkataba mpya mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe, 20. (Le10Sport – in French)

Haki miliki ya picha
Reuters

Image caption

Paris St-Germain bado haijampatia mkataba mpya mshambuliaji wa Ufaransa Kylian Mbappe

Manchester City inamnyatia beki wa Leicester na Uturuki, Caglar Soyuncu, 23. (Sunday Times – subscription required)

Kipa wa England, Jordan Pickford, 25, anasisitiza kuw awachezaji wa Everton wanamuunga mkono mkufunzi wao Marco Silva na kwamba hawako tayari kumuona akifutwa kazi. (Observer)

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na West Ham, Javier Hernandez yuko tayari kuhamia MLS. Mchezaji huyo wa kimataifa wa Mexico wa miaka 31, alijiunga na Sevilla mwezi Septemba. (LA Times)

Haki miliki ya picha
Reuters

Image caption

Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United na West Ham, Javier Hernandez yuko tayari kuhamia MLS

Tetesi Bora Jumamosi

Aliyekuwa kipenzi cha Arsenal Patrick Vieira amepuzilia mbali mpango wa kuondoka Nice- ingawa amekuwa akihusishwa na taarifa za kuchukua nafasi ya Emery. (Mirror)

Juventus wanapenda kumsajili beki wa kushoto wa Chelsea Emerson Palmieri, 25. (Calciomercato – in Italian)

Masuala ya winga wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho yameshapatiwa ufumbuzi na mchezaji huyo hatarajiwi kuondoka mwezi Januari, asisitiza Mkurugenzi wa michezo Michael Zorc. (Goal.com)

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Winga wa Borussia Dortmund, Jadon Sancho ameifungia klabu hiyo mabao tisa msimu huu

Real Madrid inafikiria kutoa ya ofa ya kiungo James Rodriguez, 28, kwa Arsenal kubadilishana na mshambuliaji raia wa Gabon Pierre-Emerick Aubameyang, 30. (El Desmarque via Calciomercato)

Inter Milan ina mpango wa kumsajili mshambuliaji Olivier Giroud,33, mwezi Januari. (Tuttosport, via Calciomercato – in Italian)

Manchester City wako kwenye mazungumzo na wakala wa kiungo wa River Plate Nicolas De La Cruz, 22. (Ole, via Sport Witness)

Haki miliki ya picha
Getty Images

Image caption

Mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez, 32, amemsifu mshambuliaji wa Chelsea Tammy Abraham akisema kuwa mchezaji huyo anaweza kuwa mbadala wake Nou Camp

Mshambuliaji wa Barcelona Luis Suarez, 32, amemsifu mshambuliaji wa Chelsea Tammy Abraham, akisema kuwa mchezaji huyo mwenye miaka 22 anaweza kuwa mwafaka kuwa mbadala wake Nou Camp. (One Football – in Spanish)

Kocha wa Tottenham, Jose Mourinho amesema Ryan Sessegnon anaweza kuwa kama beki wa kushoto wa zamani Ashley Cole, lakini anasema mchezaji huyo mwenye miaka 19, hawezi kucheza kama beki. (London Evening Standard)

Comments

More in Michezo