Connect with us

Michezo

Tanesco yatoa vipigo Shimuta – Mwanaspoti


TIMU za TANESCO zimeendelea kuwa videdea katika mashindano ya Michezo ya Mashirika ya Umma, Taasisi na Kampuni Binafsi za Tanzania (SHIMUTA).
Michezo hiyo inayoendelea jijini Mwanza inatarajiwa kuzinduliwa rasmi na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano, Samia Suluhu kesho Jumamosi uwanja CCM Kirumba.
Katika mechi za awali, timu ya soka ya Tanesco imeifunga Chuo Kikuu cha Nelson Mandela mabao 5-0.
Ushindi huo ni wa pili kwa Tanesco baada ya kushinda mechi ya kwanza dhidi ya Chuo Kikuu Tengeru na kuongoza kundi B.
Kwa upande wa mpira wa Pete, Tanesco imezifunga NHIF goli 29 – 7,  Open University goli 52 -7 na Chuo Kikuu cha Nelson Mandela nayo ikipigwa goli 46 -7.


Source link

Comments

More in Michezo