Connect with us

Michezo

Straika Mbao akerwa ligi kusimama


By MWANDISHI WETU

NAHODHA wa Mbao FC, Said Junior amesema kusimama mara kwa mara kwa Ligi Kuu Bara kunapunguza ushindani  kwenye ligi hiyo.
Baada ya mechi za leo na kesho ligi hiyo itasimama hadi mwishoni mwa mwezi ujao wakati bingwa mtetezi Simba atarejea Januari 4 mwakani kuikaribisha Yanga.
Said amesema  jinsi ligi inavyosimama mara kwa mara ndio jinsi timu nyingi  zinavyoshuka kiwango kwani kasi  ya ushindani inapunguza.
“Kama sisi tulianza vizuri baadaye tukapoteza, tukaenda ugenini tukashinda mechi mbili mfulilo na sasa unaona angalau tuko kwenye kasi nzuri lakini ligi inasimama.
“Sasa kitendo cha ligi kusimama wakati timu ndio ziko moto, zinapoozesha ile kasi ya timu kwani  mkirejea mnakuwa kama mnaaza upya.
“Mfano sasa hivi ligi inasimama kwa mwezi mzima sasa kwa hali hiyo hata kama timu ilikuwa iko kwenye  kiwango chake lakini itarudi nyuma  na hadi ligi ikirejea haitakuwa kama mwanzo,” alisema Junior.
Mbao iko nafasi ya 13 kwenye msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 14 baada ya kucheza michezo 12, imeshinda mitatu, imetoka sare michezo mitano na imepoteza minne.


Source link

Comments

More in Michezo