Connect with us

Michezo

Straika JKT Tanzania aanza tambo


By THOMAS NG’ITU

STRAIKA wa JKT Tanzania,  Adam Adam, ameanza kutamba kwamba anataka kuhakikisha anamaliza msimu wa Ligi Kuu Bara akiwa na mabao magoli 20.
Adam ambaye alifunga bao moja katika mchezo wao na Yanga, alisema anatambua ugumu wa ligi uliopo lakini anaamini kabisa kwamba kufunga kwake kumemuongezea hali ya kujiamini.
“Jambo kubwa la kumshukuru Mungu ni kufunga mara tatu mfululizo, hili linanifanya nijione kwamba morali yangu ipo juu  na kujiamini kwamba naweza kufanya tena mechi zijazo,” alisema.
Aliongeza kwa kusema “Najituma kwasababu nina malengo yangu ambayo nilianza kuyaweka tangu nikiwa Prisons, kwahiyo nazidi kujituma kadri siku zinavyokwenda,”.
Adam amefunga mfulilizo katika mechi ya Singida United, Mbeya City na Yanga.


Source link

Comments

More in Michezo