Connect with us

Michezo

Simba yaweka wazi ajenda za mkutano Mkuu


By Thomas Ng’itu

UONGOZI wa klabu ya Simba umetangaza ajenda ya mkutano wao mkuu utakaofanyika Disemba 8 mwaka huu ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere Centre.

Taarifa iliyotolewa na Mtendaji Mkuu wa Simba, Senzo Mazingiza litaja jenda hizo kuwa ni Uhakiki wa Wanachama, Utangulizi, Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Mwaka 2019, Kuhakiki Ajenda na Kuthibitisha Mukhtasari wa mkutano mkuu wa mwaka 2018.

Ajenda nyingine ni yatokanayo na mkutano mkuu wa mwaka 2018, Hotuba ya Mwenyekiti wa Mkutano, Hotuba ya Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Simba Sports Club Company Ltd.

Na ajenda ambazo zitamaliziwa ni  Uwasilishaji wa taarifa ambayo itakuwa na taarifa ya Uendeshaji wa klabu na taarifa ya Fedha kwa mwaka 2018/19 huku ajenda ya mwisho ikiwa ni kufunga mkutano.


Source link

Comments

More in Michezo