Connect with us

Michezo

Simba, Azam freshi, Mbeya City, Biashara mambo magumu


By Thomas Ng’itu

MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba pamoja na Azam FC  wameonyesha ubora wao wa kutikisa nyavu katika dakika 45 za kwanza za mechi za ligi hiyo inayoendelea kwenye viwanja tofauti nchini.
Simba wpao uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam wakikaribishwa na Ruvu Shooti wakati Azam nao wapo ugenini uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza ambapo kila  timu imekwenda mapumziko ikiwa inaongoza bao 1-0.
Bao la Simba lilifungwa na Miraji Athuman dakika ya 39 ambaye amefikisha mabao matano sasa akiunganisha krosi ya Shomari Kapombe wakati Azam ilipata bao lake kupitia beki wao  Yakubu Mohamed dakika ya 18 akipiga shuti kali nje ya boksi.
Matokeo mengine katika kipindi cha kwanza, Mbeya City ambao ni wenyeji wa Singida United uwanja wa Sokoine timu hizo zimeenda mapumziko zikiwa hazijafungana sawa na Biashara United dhidi ya Mtibwa Sugar.
Hivyo kunawafanya Simba na Azam kuwa ndio timu pekee ambazo zimeweza kupata goli dakika 45 za kipindi cha kwanza kaik mechi nne zinazochezwa leo Jumapili.


Source link

Comments

More in Michezo