Connect with us

Michezo

Shiboub, Kagere waibuka mazoezini – Mwanaspoti


By Thobias Sebastian

WACHEZAJI wa Simba waliokuwa katika majukumu ya timu zao za Taifa wameonekana leo Ijumaa kwenye mazoezini kasoro mmoja pekee.
Mchezaji aliyekosekana ni kiungo wa timu ya Taifa ya Zambia, Cletous Chama ambaye hakuwa katika sehemu ya kikosi hicho kilichofanya mazoezi.
Ukiachana na hilo katika mazoezi ya siku mbili ambayo Simba waliyofanya walimkosa kiungo Sharaf  Eldin Shiboub na straika Meddie Kagere ambao mbali ya kuwa katika majukumu ya timu za taifa lakini walikuwa na matatizo yao binafsi.
Katika mazoezi ya jana Alhamis, Simba walifanya uwanja Uhuru kocha Patrick Aussems alisema Kagere alikuwa na matatizo ambayo yanaweza kumfanya kukosa mechi ya kesho Jumamosi dhidi ya Ruvu Shooting.
“Kagere amekosa mazoezi ya jana, kutokana na matatizo yake binafsi mbali ya kumaliza majukumu ya timu yake ya taifa,” alisema Aussems.
Katika mazoezi ya leo asubuhi yaliyofanyika viwanja  vya Gymkhana Kagere alikuwa sehemu ya wachezaji wa Simba na kufanya mazoezi aina mbili.
Mbali ya Kagere kurejea Shiboub nae alikuwepo akionekana kuwa fiti na kufanya mazoezi kama wachezaji wengine.


Source link

Comments

More in Michezo