Connect with us

Michezo

Samatta, Salah, Mane wawania tuzo Mwanasoka bora Afrika


By THOBIAS SEBASTIAN

Dar es Salaam. Nahodha wa Taifa Stars na klabu KRC Genk, Mbwana Samatta ameingia katika orodha ya wachezaji 30 wanaowania tuzo ya mwanasoka bora wa mwaka wa Afrika.

Kwa mujibu wa orodha iliyotolewa na CAF imetaja majina ya wachezaji 30 wanaonia tuzo hiyo ikiwa na wachezaji wengi wanaocheza soka barani Ulaya.

Samatta ambaye wiki hii amesakamwa kwenye mitando ya kijamii kwa kushinda kucheza vizuri akiwa Stars ndiye Mtanzania pekee aliyeiongoa katika kinyang’anyiro hicho ikiwa ni kwa mara tatu sasa.

Samatta ametajwa katika orodha hiyo baada ya kuisaidia klabu yake ya KRC Genk kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Ubelgiji msimu uliopita pamoja na kufunga mabao 30 katika mashindano yote.

Katika tuzo hiyo Samatta anategemea kupata ushindani mkali kutoka kwa Mohamed Salah wa Misri, Sadio Mane wa Senegal ambao waliiongoza Liverpool kutwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa.

Pia, Samatta atakuwa na ushindani na Riyad Mahrez aliyeiongoza Algeria kutwaa ubingwa wa Kombe la Mataifa Afrika pamoja na kuiongoza Manchester City kutetea taji la Ligi Kuu England.

Advertisement

Katika mbio za kuwania tuzo hiyo pia yupo mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang wa Gabon na Arsenal aliyekuwa mfungaji bora wa Ligi Kuu England.

Mbali ya Samatta ni mtanzania wa kwanza aliyeshinda tuzo mwanasoka bora Afrika kwa wanaocheza ndani mwaka 2015, akiwa na TP Mazembe kabla ya kujiunga na Genk.

Tuzo ya Mwanasoka bora mwaka wa Afrika

·      Achraf Hakimi (Morocco & Borussia Dortmund)

·      André Onana (Cameroon & Ajax)

·      Baghdad Bounedjah (Algeria& Al-Sadd)

·      Carolus Andriamatsinoro (Madagascar & Al Adalah)

·      Denis Onyango (Uganda & Mamelodi Sundowns)

·      Eric Maxim Choupo-Moting (Cameroon & Paris Saint-Germain)

·      Ferjani Sassi (Tunisia & Zamalek)

·      Hakim Ziyech (Morocco & Ajax)

·      Idrissa Gueye (Senegal & Paris Saint-Germain)

·      Ismail Bennacer (Algeria & AC Milan)

·      Jordan Ayew (Ghana & Crystal Palace)

·      Kalidou Koulibaly (Senegal & Napoli)

·      Kodjo Fo Doh Laba (Togo & Al Ain)

·      Mahmoud Hassan”Trezeguet” (Egypt & Aston Villa)

·      Mbwana Samatta (Tanzania & Genk)

·      Mohamed Salah (Egypt & Liverpool)

·      Moussa Marega (Mali & Porto)

·      Naby Keita (Guinea & Liverpool)

·      Nicolas Pepe (Côte d’Ivoire & Arsenal)

·      Odion Ighalo (Nigeria & Shanghai Shenhua)

·      Percy Tau (South Africa & Club Brugge)

·      Pierre-Emerick Aubameyang (Gabon & Arsenal)

·      Riyad Mahrez (Algeria & Manchester City)

·      Sadio Mane (Senegal & Liverpool)

·      Taha Yassine Khenissi (Tunisia & Esperance)

·      Thomas Teye Partey (Ghana & Atlético Madrid)

·      Victor Osimhen (Nigeria & Lille)

·      Wilfred Ndidi (Nigeria & Leicester City)

·      Wilfried Zaha (Côte d’Ivoire & Crystal Palace)

·      Youcef Belaili (Algeria & Ahli Jeddah)


Source link

Comments

More in Michezo