Connect with us

Michezo

Sahare wafurahia haki Jamhuri – Mwanaspoti


By Juma Mtanda

KOCHA wa Sahare All Stars Fc ya Tanga, Shekue Swaleh amesema moja ya viwanja bora na vyenye kutoa haki Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara ni Jamhuri mjini Morogoro. 
Akizungumza na Mwanaspoti mjini hapa, Swaleh alisema Uwanja wa Jamhuri umekuwa tulivu na waamuzi wanacheza kwa kufuata kufuata sheria 17 za soka bila upendeleo tofauti na meeneo mengine.
Alisema katika mchezo wao dhidi ya wenyeji Mawenzi Market SC, mwamuzi wa mchezo huo alifuata sheria 17 za soka bila kupendelea wenyeji jambo ambalo sio rahisi kutokea katika viwanja vingine.
“Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara kumekuwa na desturi ya timu mwenyeji kupata matokeo kwa lazima wanapokuwa uwanja wa nyumbani, lakini Morogoro ni tofauti kabisa,” alisema Swaleh.
Swaleh alisema waamuzi wa mchezo wao na Mawenzi Market SC, waamuzi walichezesha mchezo huo kwa kufuata haki na makosa yalijitokeza yalikuwa makosa ya kibinadamu tofauti na viwanja vingine.
Mchezo huo ulichezeshwa na mwamuzi wa kati, Saidi Pambalelo wa Dar es Salaam akisaidiwa na mshika kibendera nambari moja, Hashim Mgumba na Kelvin Machanza na ulimalizika kwa sare ya bila kufungana.
Swaleh alisema katika michezo miwili ya timu ya Sahare Ally Stars iliyopita, kabla ya kucheza na Mawenzi Market Sc walipoteza ugenini mbele ya wenyeji akidai vipigo walivyopata vilitokana na wapinzani wao kubebwa.


Source link

Comments

More in Michezo