Connect with us

Rubani aliyesababisha ajali iliyoua waandishi Kenya alilewa

Nairobi, Kenya. Ripoti ya uchunguzi ya tukio la ajali ya helkopta iliyotokea katika Ziwa Nakuru, Kenya imebaini rubani alilewa.

Ajali hiyo ilihusisha helkopta ya Flex Air Limited, aina ya AS 350 B3 yenye usajili namba 5Y-NMJ ambayo ilibeba timu ya mawasiliano ya Seneta wa Nakuru, Susan Kihika.

Helkopta hiyo ilidondoka katika Ziwa Nakuru Oktoba 21, 2017 saa 12:37 asubuhi na kuua watu wote wanne akiwamo rubani wake.

Ripoti hiyo iliyotolewa jana na Waziri wa Uchukuzi wa Kenya, James Macharia pamoja na mambo mengine imebaini helkopta hiyo ilidondoka kwenye ziwa baada ya rubani kupoteza uelekeo kutokana na kitendo chake cha kunywa pombe.

Ripoti hiyo ilimtaja Kapteni Apollo Malowa ambaye ndiye alikuwa rubani wa helkopta hiyo kuwa alishindwa kuidhibiti kutokana na ulevi kupindukia.

Miili ya marehemu waliotokana na ajali hiyo ambayo ni Kapteni Malowa, Veronicah Muthoni na Anthony Kipyegon walipatikana baada ya siku 25 wakati Sam Gitau na John Mapozi hawajapatikana mpaka sasa.

Advertisement

“Ilichukua zaidi ya siku 25 kupata miili mitatu ya watu kwenye helkopta hiyo. Utafutaji wa miili mingine haukufaulu hata baada ya shughuli za uokozi kuongezwa kwa miezi mitatu baadaye,” ilisisitiza ripoti hiyo.

Rubani huyo wa helkopta alikuwa mhitimu mpya wa miaka 22 wa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Rift Valley.

Comments

More in