Connect with us

Michezo

Prisons yapigia hesabu nne bora


By Olipa Assa

KATIBU wa Prisons, Ajibu Kifukwe amesema wachezaji wao ndio wana deni la kuhakikisha wanaifikisha timu kwenye malengo waliojiwekea kwamba wanatekelezewa mahitaji yao kwa wakati.

Anasema viongozi wamekuwa wepesi kuwajibika na kuhakikisha hawawi sababu ya timu kufanya ovyo na kusisitiza kwamba kazi imebaki kwa wachezaji kufanya upande wao.

Ametaja malengo yao kwamba ni kuhakikisha hawabanduki kwenye nne bora na sasa wapo nafasi ya tatu, hivyo amewataka wachezaji kulinda nafasi hiyo.

“Najua si kazi rahisi ligi ina ushindani mkubwa sana, kikubwa wapambane kuona wanatufikisha kwenye malengo yetu ya msimu,”

“Tupo bega kwa bega na kila wanachokuwa wanakihitaji kutoka kwetu, pia kujua kocha ana mahitaji gani kutoka kwetu ili tuyatekeleze ndani ya muda sahihi,”amesema.


Source link

Comments

More in Michezo