Connect with us

Michezo

Nonga ambipu Kagere – Mwanaspoti


By Olipa Assa

STRAIKA wa Lipuli FC  ya Iringa, Paul Nonga anakuja kwa kasi katika kuzifumania nyavu, yupo nyuma bao moja dhidi ya Meddie Kagere wa Simba anayeongoza kwa mabao sita.
Nonga amesema moto aliouwasha hawezi kuuzima na akitaja malengo yake kwamba anataka kupambania kiatu cha dhahabu ambacho kimekwenda kwa wachezaji wa kigeni misimu miwili mfululizo.
Amesema anatamani kila mechi awe anafunga ili kutimiza ndoto yake ya msimu huu na kwamba anapata morali akiona wachezaji wa kigeni wanakuja kwa kasi.
“Kikubwa naomba Mungu anijalie uzima, najituma kwenye mazoezi binafsi ili kuona nafanya kitu msimu huu, binafsi naamini wazawa tunaweza tukafanya mambo makubwa,”
“Nina wivu wa maendeleo sina maana kwamba wageni wanapofanya vizuri nawachukia, lengo langu nahitaji tuibue ushindani wa hali ya juu ili ligi yetu iwe na mvuto mkubwa,”amesema.


Source link

Comments

More in Michezo