Connect with us

Michezo

Mwambusi abwaga manyanga Mbeya City


By Thomas Ng’itu

KOCHA  wa Mbeya City, Juma Mwambusi ameandika barua ya kujiuzuru kuifundisha timu hiyo kutokana na mwenendo mbovu wa matokeo kwenye mechi za Ligi Kuu Bara.

Katika kikao chake kilichofanyika leo Jumamosi pamoja na Bodi ya Mbeya City, bodi hiyo imeridhia ombi la kocha huyo kujiuzuru.

Taarifa hiyo ilieleza kwamba Mwambusi aliwasilisha ombi la kujiuzuru tangu Novemba 26 mwaka huu kwa maslahi mapana ya klabu kufutuatia mwenendo usioridhisha wa timu tangu kuanza.
 “Katika kipindi hiki cha mpito Bodi yetu imemkabidhi timu Kocha Msaidizi Mohamed Kijuso huku mchakato wa kumtafuta kocha mkuu ukiendelea” ilisema taarifa hiyo iliyotolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Mbeya, James Kasusura.

Taarifa hiyo ilieleza zaidi kwamba Bodi inamshukuru Mwambusi kwa mchango wake mkubwa kwa maendeleo ya timu na bado inahitjai ushauri na uzoefu wake katika tasnia ya michezo.

Mbeya City inashika nafasi ya 18 ikiwa na pointi nane katika michezo 12 waliyocheza.


Source link

Comments

More in Michezo