Connect with us

Michezo

Mwakinyo ashangaa Diamond, AliKiba kushindwa kumsapoti


By Mwandishi Wetu

Dar es Salaam. Bondia mahiri wa Tanzania, Hassan Mwakinyo ameshangazwa na jinsi wasanii wakubwa wa Tanzania akiwemo Diamond na AliKiba kushindwa kuwasapoti.

Mwakinyo kesho Ijumaa atapanda ulingoni kuzichapa na Arnel Tinampay wa Ufilipino katika pambano lisilo la ubingwa la uzani wa Super Welter litakalofanyika kwenye Uhuru jijini Dar es Salaam.

Mwakinyo amesema ni jambo linaloumiza kuona wakipata sapoti ndogo katika mapambano kama haya ya ngumi ilihali watu wote wana weza kufanya hivyo ili kuipaisha nchi yetu.

“Kuna sapoti ndogo sana hapa nchini kwetu kwani ukiangali sisi ni mabondia ambao tunamsikiliza Diamond, AliKiba, Ommy Dimpozi na wengine wengi na mara kwa mara tunacheza nyimbo zao, lakini hatuwaoni katika matukio kama haya.

“Ukizingatia sisi tunafanya vitu kwa niaba ya Watanzania na tunasapoti kazi zao na wao ilipaswa wasapoti kazi zetu kwa sababu tuko pamoja kulijenga taifa,” alisema Mwakinyo.

Nchi zilizoendelea kama Marekani wasanii wakubwa   kama Kanye West, R.Kelly na wengine wamekuwa wakihudhuria mapambao mbalimbali ya ngumu na hata michezo mingine ikiwa ni kusapoti mabondia kutoka nchi zao.

Advertisement


Source link

Comments

More in Michezo