Connect with us

Michezo

Mhilu wanakaba hadi kivuli chake


By Charity James

MSHAMBULIAJI wa Kagera Sugar, Yusuf  Mhilu amefunguka ugumu anaokutana nao kutoka kwa mabeki wakati anapambana kusaka nafasi ya kuifungia timu yake kuwa amekuwa akikamiwa sana.
Mhilu hadi sasa ameingia kambani mara tano katika michezo 11 waliyocheza na kukusanya pointi 23 zilizowapandisha kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara.
Mhilu amesema timu nyingi wanazokutana nazo zimejua wachezaji ambao wanaipa timu yao matokeo hivyo wamekuwa wakiwabana ili kuwazuia wasifunge.
“Hadi sasa mimi ndiye kinara wa upachikaji wa mabao kwa timu yangu hivyo nim ekuwa nikikabwa mno lakini kutokana na kuwa na mipango na kuhakikisha naipa timu yangu matokeo nimekuwa nikipambana zaidi kwa kila mbinu na hatimaye kupata nafasi ya kufunga.
“Kitu kikubwa kinachonibeba ni jitihada zangu binafsi kuhakikisha najiweka fiti lengo ni kuhimili mikikimikiki ya mabeki ambayo nimekuwa nakutana nayo, nakabwa hata na watu wawili hili nisingekuwa na pumzi basi naamini uwezo wa kuendelea kupambana kutengeneza nafasi sidhani kama ningekuwa nao,” alisema.


Source link

Comments

More in Michezo