Connect with us

Michezo

Mchezaji Mbeya City akamatawa na dawa za kulevya


By Godfrey Kahango, Mbeya

BEKI wa zamani wa Mbeya City, Geogratius Julius (27) ambaye ni mkazi wa Soweto jijini hapa anashikiliwa na Polisi Mkoa wa Mbeya baada ya kutuhumiwa kwa kukamatwa akiwa na dawa zidhaniwazo kuwa ni za kulevya aina ya Heroine kete 27.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya Ulrich Matei amesema kwamba polisi waliokuwa doria walikamata Julius akiwa na dawa hizo ambazo alikuwa amezificha kwenye mfuko wa suruali aliyokuwa ameivaa.
Alisema wamekata Novemba 20 mwaka huu muda wa saa 21:00 usiku na baada ya mtuhumiwa kuhojiwa alidai dawa hizo alipewa na mtu mmoja mkazi wa Mafiati jijini hapa.
Matei alisema baada ya hapo Jeshi la Polis lilianza msako wa kumtafuta mtu huyo aliyetajwa na Julius na leo Jumatatu alfajiri walifanikiwa kumdaka mtuhumiwa huyo eneo la Mwambene Kata ya Ilomba jijini hapa.


Source link

Comments

More in Michezo