Connect with us

Michezo

Mbrazil wa Simba awaacha hoi mashabiki


By Olipa Assa na Thobias Sebastian

BEKI wa Simba, Mbrazil Tairone Santos amewaacha hoi mashabiki baada ya kufunga bao kwa kichwa dakika ya 47 kisha kutoka mbio kwenda kushangilia na mashabiki.
Santos hakuishi hapo baadae alikimbilia kwenye benchi la ufundi ambapo alikwenda kukumbatiana na Deo Kanda kisha kocha wake, Patrick Aussems.
Bao la Simba limepatikana baada ya Mkenya Francis Kahata kuchonga kona na Santos kuiunga kwa kichwa.
Mashabiki baadhi walijikuta wanacheka aina ya ushangiliaji wa Santos huku wengine wakiungana naye kushangilia.
Simba ambayo inaonekana kuwa mbabe wa Ruvu Shooting  msimu ulioisha mzunguko wa kwanza iliibuka na ushindani wa mabao 5-0 na wa pili mabao 2-0, mechi inayoendelea muda huu Uwanja wa Uhuru inaongoza mabao 2-0.


Source link

Comments

More in Michezo