Connect with us

Michezo

Mastaa kuukosa Usiku wa Ulaya


Wakati mechi nane za hatua ya makundi katika Ligi ya Mabingwa Ulaya zikisubiriwa kuchezwa leo, idadi kubwa ya nyota wa klabu mbalimbali watakosekana katika vikosi vya timu zao kutokana na sababu tofauti.
Real Madrid ambayo inahitajika kupata ushindi dhidi ya PSG leo ikiwa nyumbani Uwanja wa Santiago Bernabeu na kuombea Club Brugge isipate ushindi dhidi ya Galatasaray, itawakosa nyota wake watano kutokana na changamoto ya majeruhi na sababu za kiufundi.
Kinda Vinicius Jr na Nacho watakosekana kutokana na sababu za kiufundi wakati nyota watakaokosekana kutokana na majeraha ni James Rodriguez na Marco Asensio wanaouguza majeraha ya goti pamoja na Lucas Vazquez mwenye majeraha ya kidole.
Kwa upande wa PSG, nyota watakaosekana ni Choupo-Moting anayesumbuliwa na maumivu ya mgongo, Ander Herrera (nyama za misuli) na Layvin Kurzawa ambaye atakosekana kwa sababu ambazo hazijawekwa wazi.
Yunus Akgün wa Galatasaray ataukosa mchezo dhidi ya Club Brugge kutokana na kutumikia adhabu ya kadi lakini pia klabu hiyo itawakosa Radamel Falcao (kisigino), Christian Luyindama na Florin Andone (goti) pamoja na Steven Nzonzi aliyesimamishwa wakati wapinzani wao watawakosa Matej Mitrovic anayesumbuliwa na enka na Ruud Vormer aliyesimamishwa.
Ben Davies (misuli), Hugo Lloris (mkono), Michael Vorm (kifundo) na Erik Lamela (nyama) hawatakuwa sehemu ya kikosi cha Tottenham inayoialika Olympiacos ambayo itamkosa Pape Cisse.
Niklas Sule na Lucas Hernandez watakosekana katika kikosi cha Bayern Munich kitakachocheza dhidi ya Crvena Zvezda wakati Manchester City itawakosa nyota watano huku wawili wengine wakiwa kwenye hatihati pale itakapokuwa inavaana na Dinamo Zagreb.
Leroy Sane, Aymeric Laporte na Zichenko watakosena kutokana na majeraha ya goti wakati Sergio Aguero anauguza maumivu ya misuli lakini pia watamkosa kipa Claudio Bravo ambaye anatumikia adhabu. Walio kwenye hatihati ni David Silva (misuli) na Rodrigo (nyama za paja).


Source link

Comments

More in Michezo