Connect with us

Michezo

Mabeki Ruvu wamkalisha Kagere – Mwanaspoti


By Olipa Assa

STRAIKA wa Simba, Meddie Kagere ana kazi kubwa ya kuendelea kuzifumania nyavu baada ya washambuliaji wengine kuja kwa kasi.
Katika mechi ya leo Jumamosi iliyopigwa Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam timu yake ikicheza na Ruvu Shooting, Kagere ametumia dakika 75 kusaka bao bila mafanikio.
Tangu Oktoba, Ligi Kuu ya Vodacom  (VPL) ilipoanza Kagere ndiye kinara wa mabao licha ya kuwepo dalili za kupinduliwa kutokana na washambuliaji kama Paul Nonga kufikisha mabao saba.
Ukiachana na Nonga wa Lipuli kumiliki mabao saba washambuliaji wengine wenye mabao sita ni Miraji Athuman (Simba) na Daruesh Saliboko (Lipuli FC).
Mabeki wa Ruvu Shooting wameonekana kumkaba Kagere ambaye ameshindwa kufurukuta mbele yao.






Source link

Comments

More in Michezo