Romelu Lukaku hatimaye asajiliwa Man U – Julai 4, 2024

KWA mujibu wa tetesi za usajili wa kimataifa, Manchester United ipo tayari kujaribu kumsajili tena mshambuliaji Romelu Lukaku kutoka Chelsea iwapo itashindwa kufikia dili na Joshua Zirkzee inayomlenga zaidi. (Calciomercato.it, Italy)

Romelu Lukaku, aliyezaliwa tarehe 13 Mei 1993 huko Antwerp, Ubelgiji, ni mshambuliaji hodari anayejulikana kwa nguvu zake za kimwili, kasi, na uwezo wake wa kufunga mabao.

Alikuza kazi yake ya soccer katika klabu ya Anderlecht huko Ubelgiji, ambapo mafanikio yake mazuri yalimsaidia kuhamia Chelsea mwaka 2011. Hata hivyo, Lukaku alikumbana na changamoto za kupata muda wa kutosha wa kucheza Chelsea na baadaye akafanikiwa kwenda kwa mkopo West Bromwich Albion na Everton.

Akiwa Everton, Lukaku alikuwa na mafanikio makubwa, akawa miongoni mwa wafungaji bora katika Ligi Kuu ya England na kuvunja rekodi za klabu.

Mafanikio yake makubwa yaliivutia Manchester United, ambao walimsajili mwaka 2017 akichangia kufunga mabao mengi United.

Mwaka 2019, Lukaku alihamia Inter Milan, ambapo alipata mafanikio makubwa zaidi chini ya kocha Antonio Conte. Alikuwa sehemu muhimu katika ushindi wa Serie A wa Inter msimu wa 2020-2021, ukikatiza utawala wa Juventus nchini Italia.

Nguvu zake za kimwili, uwezo wake wa kiufundi, na umahiri wake wa kufunga mabao vilimfanya kuwa mmoja wa wachezaji muhimu katika safu ya ushambuliaji ya Inter.

Kupitia kazi yake ya soka, Lukaku ameiwakilisha timu ya taifa ya Ubelgiji kwa mafanikio makubwa, akishiriki katika mashindano makubwa kama Kombe la Dunia la FIFA. Amekuwa miongoni mwa wafungaji bora na wachezaji muhimu wa Ubelgiji.

Safari ya Lukaku katika soka inaonyesha uvumilivu wake, uwezo wake wa kubadilika, na uwezo wake mkubwa wa kufunga mabao, kumtambulisha kama mmoja wa washambuliaji mahiri zaidi katika soka ya Ulaya.

Katika tetesi yingine Benfica imekataa maombi ya Man Utd na Paris Saint-Germain ya pauni mil 59 kumsajili kiungo wake Joao Neves huku klabu hiyo ya Ureno ikiwa imejiandaa tu kufanyia biashara kipengele cha kuachiwa cha mchezaji huyo cha pauni mil 102. (Correio da Manha, Portugal)

Klabu za Arsenal, Chelsea, Liverpool, Manchester City na Manchester United zimewasiliana na kiungo wa PSG, Xavi Simons, lakini ameweka wazi kwamba hataki kucheza Ligi Kuu England msimu ujao. (TBR Football)

Newcastle United imeionya Liverpool kwamba itagharimu angalau pauni mil 100 kumsajili winga Anthony Gordon majira haya a kiangazi. (Football Insider)

Kiungo wa Scotland Scott McTominay anahitajika Fulham, ambayo inatarajiwa kuwasilisha ombi Man Utd hivi karibuni. (ManchesterWorld)

Conor Gallagher anasita kuhamia Midlands kujiunga na Aston Villa na sasa anasubiri uwezekano wa mkataba mpya katika klabu ya Chelsea. (The Telegraph)

Bologna imekataa ombi la Arsenal la pauni mil 40 kwa ajili ya kumsajili beki wa kati Riccardo Calafiori. Chelsea pia ina nia kumsajili mchezaji huyo wa kimataifa wa talia. (Corriere dello Sport, Italy)

Al Nassr imekubaliana vipengele binafsi na golikipa wa Manchester City, Ederson. (Gianluigi Longari, Italy)

Liverpool imefanya mawasiliano kuhusu dili la kumsajili mchezaji huru Adrien Rabiot, lakini kwa sasa kiungo huyo wa kifaransa anasikiliza tu nia ya Real Madrid. (Calciomercato, Italy)

Barcelona inafikiria kumsajili tena beki wa kulia wa Tottenham Hotspur, Emerson Royal, anayeonekana kuwa mbadala iwapo itashindwa kumshawishi kurejea Joao Cancelo kutoka Man City. (CaughtOffside)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *