Connect with us

Michezo

Kilimanjaro Queens, Uganda wagawana ubora


By Doris Maliyaga

MAKIPA wa timu tofauti kwenye michuano ya Cecafa ya wanawake inayoendelea jijini Dar es Salaam wametikishwa mara 74 hadi sasa ambapo michuano hiyo kesho Jumamosi itaendelea hatua ya nusu fainali.
Katika michuano hiyo, jumla ya hat-trick nane zimefungwa kwenye Uwanja wa yAzam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam ambako ndiko mashindano hufanyika.
Tanzania Bara ‘Kiliamnjaro Queens’ ndio vinara wa mabao wamefunga 20, Kenya 17, Uganda wa tatu 14, Burundi 10, Ethiopia manane na Sudan Kusini matano, Zanzibar na Djibouti hawajafunga.
Kilimanjaro Queens iliipiga Sudan Kusini mabao 9-0, Zanzibar 7-0 na Burundi 4-0. Kenya iliishinda Djibouti 12-0, Uganda 3-0 na Ethiopia 2-0.
Uganda waliifunga Djibouti 13-0, Ethiopia 1-0 wakafungwa na Kenya.  Burundi walikuwa wazee wa tanotano wameichapa Zanzibar 5-0  na Sudan Kusini 5-0.
Ethiopia waliishinda Djibouti 8-0, wakafungwa na Kenya na Uganda,  wakati Sudan Kusini iliichapa Zanzibar 5-0, wakafungwa na Tanzania Bara na Burundi.
Hii inaonyesha namna ushindani ulivyokuwa mkubwa ndani ya michuano hiyo.
Kocha wa Kilimanjaro Queens, Bakari Shime ‘Mchawi Mweusi’ alisema, kwake idadi ya mabao si ishu anachoangalia ni namna gani kikosi chake kinacheza uwanjani.
Upande wa hat-trick vinara ni Uganda wamefunga Nasuuna Hasifai,  Ikwaput Fadhila na Narukenge Juliet,  Kenya wana mbili, Mwanalima na Merci Airo,  Kilimanjari Queens ni Mwanhamisi Omary ‘Gaucho’, Ethiopia imefungwa na Erehima Zerega na Burundi Niyonkuru Sadrine.


Source link

Comments

More in Michezo