Connect with us

Michezo

Keisha aingia mapema kumshuhudia Mwakinyo


By OLIPA ASSA

MSANII wa muziki wa Bongo Flava, Keisha ni miongoni mwa watu maarufu waliofika kushuhudia pambano la Hassan Mwakinyo na Arnel Tinamay raia wa Ufilipino.
Keisha ambaye amewahi kutamba na vibao mbalimbali ikiwemo Nioe, Nipe raha na Nalia amefika mapema kusapoti pambano hilo.
Akionekana yupo tayari kushuhudia pambano hilo, akifurahia na muziki unaopigwa kunogesha pambano hilo.
Akiwa amevalia nguo za Chama Cha Mapinduzi (CCM), yupo makini kufuatilia kila linaloendelea Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.
Anashuhudia  pambano la utangulizi kati ya Aziz Juma na Hemed Mremba la raundi nne ambalo linasimamiwa na Emmanuel Mlundwa.


Source link

Comments

More in Michezo