Connect with us

Michezo

Kagera Sugar yapotea nyumbani – Mwanaspoti


By Saddam Sadick, Mwanza

KAGERA Sugar imekubali kulala nyumbani kwa kipigo cha mabao 3-1 dhidi ya Mtibwa Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa uwanja wa Kaitaba.

Kagera Sugar ambao walikuwa na mwendelezo mzuri kwenye ligi, leo hawakuamini kilichowatokea kwenye uwanja wao kutokana na kupoteza mechi hiyo.

Kagera Sugar ndio walitangulia kupata bao dakika ya 39 kupitia Awesu Awesu na kuwafanya kwenda mapumziko wakiwa mbele kwa bao 1-0 dhidi ya wapinzani wao  Mtibwa Sugar kutoka mkoani Morogoro.

Kipindi cha pili Mtibwa Sugar walipambana na kutengeneza mashambulizi kadhaa ambapo wakati Juma Nyosso wa Kagera Sugar akijaribu kuokoa moja ya hatari alijikuta anaukwamisha mpira wavuni na kuufanya mchezo kuwa sare ya bao moja.

Kuingia kwa bao hilo kuliipa nguvu zaidi Mtibwa Sugar kwa kulisakama zaidi lango la Kagera Sugar na dakika ya 78 Haruna Chanongo akaipatia la pili na dakika ya 90 akaiongezea tena la pili na kukamilisha idadi ya mabao hayo na kuihakikishia pointi tatu timu yake.

Kupoteza mchezo huo kwa Kagera Sugar inafikisha mechi ya tatu kukwama nyumbani ikiwa ni dhidi ya Simba bao 3-0 na JKT Tanzania iliyowalaza 1-0.

Advertisement

Alliance FC 0 – 5 Azam FC

Mbeya City 1- 2 Mwadui FC

Kagera Sugar 1- 3 Mtibwa Sugar

Biashara United 1-0 Lipuli FC

JKT Tanzania 2-1 Ruvu Shooting


Source link

Comments

More in Michezo