Connect with us

Michezo

Gadiel awaza makubwa VPL – Mwanaspoti


By OLIPA ASSA

BEKI wa Simba, Gadiel Michael anautazama msimu huu kama utakuwa wa mafanikio kuonyesha kiwango cha juu, akitoa sababu kwamba ligi imekuwa ngumu hivyo inayohitaji kujituma.
Gadiel amesema anaamini katika jambo gumu akili inatakiwa kutumika kubwa hivyo ugumu wa ligi anauchukulia kama atajituma zaidi mazoezini.
“Asikuambie mtu ligi ni ngumu hii inasaidia mchezaji kujituma kwa bidii kufanya kazi yake kuhakikisha hawaangushi waliomwajiri,”
“Lengo langu ni kuhakikisha nakuwa na mchango mkubwa Simba ambao wamenipa ajira na kuniamini kwamba nitaweza kufanya maajabu,”amesema.
Amesema licha ya kuwa ligi ni ngumu lakini anafurahia ushindani umeanzia ndani ya timu ambapo mpinzani wake  Mohamed Hussei ‘Tshabalala’ kuwa na kiwango cha juu.
“Nina ndoto za kufika mbali, huwa nafurahia kuona ninayeshindana naye kwenye namba anakuwa na kiwango kikubwa, kinachokuwa kinanifanya mimi kuwa makini zaidi,”amesema.


Source link

Comments

More in Michezo