Connect with us

Michezo

Emery hafukuzwi kisa Pauni 4milioni


LONDON, ENGLAND . IMEFICHUKA kuwa Arsenal wamechelewesha kumfuta kazi Unai Emery kabla ya msimu kumalizika wakikwepa kulipa fidia ya Pauni 4 milioni.

Mhispaniola huyo yupo kwenye presha kubwa huko Emirates baada ya timu kufanya ovyo na hawajashinda mechi yoyote tangu Oktoba 24, huku Oktoba 6 ndiyo ilikuwa mara ya mwisho kushinda kwenye Ligi Kuu England.

Sare ya kutoka kwa Southampton Jumamosi iliyopita ilimweka kwenye wakati mgumu zaidi Emery, lakini kumbe Arsenal wanaogopa kumfukuza sababu tu hawataki kulipa fidia ya Pauni 4 milioni.

Kwamba wanachosubiri ifike mwisho wa msimu ambapo, ataondoka bila ya kuwaingiza kwenye gharama yoyote ile.

Kocha Emery mwenyewe wala hana presha na kusema:

“Klabu inanisapoti kwa kila kitu na mimi nawajibika pia. Nasubiri kuona mambo yatakavyokuwa.”

Advertisement


Source link

Comments

More in Michezo