Connect with us

Michezo

Buswita ndani ya uzi wa Polisi Tanzania


By YOHANA CHALLE

MARA baada ya kusaini mkataba wa miezi sita kuitumikia Polisi Tanzania, Pius Buswita ameweka wazi malengo yake kwamba ni kuhakikisha anaisaidia timu yake kutimiza malengo kwenye mashindano mbalimbali watakayoshiriki.
Buswita  alisema ni faraja kwake kurudi nyumbani baada ya muda mrefu kushindwa kuonekana uwanjani, hivyo wapenzi wa timu hiyo watarajie mambo makubwa kutoka kwake.
“Kila kazi ina changamoto zake, najua ni mapito tu niliyopita kwa muda ambao sikuonekana baada ya kuachana na Yanga, nilikwenda Rwanda kujiunga na moja ya timu huko lakini mahusiano yetu hayakuwa mazuri hadi kufika hatua ya kuachana nao na kurejea nyumbani kwa sasa,” alisema Buswita.
Afisa Habari na Mawasiliano wa timu hiyo, Frank Lukwaro alisema wameamua kumsajili mchezaji huyo kutokana na uwezo wake mkubwa kwenye soka kwa miaka ya nyuma kabla ya siku za karibuni mambo kumwendea vibaya.
“Tunaamini ataisaida timu kufanya vizuri kwa kushirikiana na wachezaji wenzake, lakini uzoefu wake kwenye soka la Tanzania ni moja ya vitu ambavyo vimetushawishi kufanya naye kazi kwa miezi iliyobaki ya Ligi Kuu, mambo yakiwa mazuri basi tunaweza tukaendelea naye misimu inayofuata,” alisema Lukwaro.
Aliongeza baada ya kumalizana na Buswita juzi Alhamisi, zoezi hilo litaendelea wakati wa dirisha dogo la usajili kwa wachezaji litakapofunguliwa Desemba 15 kwa kuongeza nguvu kikosi chao ili kuendelea kuwa na makali kupambana na kila michezo itakayokua mbele yao ya ligi na mashindano mengine watakayoshiriki.
Majeraha ya kila mara ndio sababu yaliyomfanya mchezaji huyo kukosa nafasi ndani ya kikosi cha Yanga iliyokuwa chini ya Mwinyi Zahera ambaye mara nyingi alikuwa akiishia benchi kuuguza majeraha.
Yanga ilimsajili Buswita kutoka Mbao FC msimu wa 2017/18 kwa mkataba wa miaka miwili na baadaye kukutwa na kosa la kusaina timu mbili, Simba na Yanga kabla ya Kamati ya Sheria, Katiba na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka nchini (TFF) kuamua kwamba mchezaji huyo arudishe pesa aliyochukuwa Simba.
Buswita alianza soka ya ushindani Polisi Mara (Biashara United) aliyoitumikia kwa miaka mwili na baadaye kutua Mbao FC mwaka 2015 aliyoichezea mwaka mmoja na kuisaidia kupanda daraja hadi Ligi Kuu Bara.


Source link

Comments

More in Michezo