Connect with us

Michezo

Bayern Munich wateta na wakala wa Leroy Sane


BAYERN Munich wamerudi rasmi tena katika mbio za kumchukua winga mahiri wa Manchester City, Leroy Sane na tayari wamekutana na wakala wa staa huyo wa kimataifa wa Ujerumani, Giovanni Branchini kwa ajili ya kujadili uhamisho huo.

Kwa muda mrefu Sane ni majeruhi na Bayern haitazamiwi kumchukua katika dirisha la Januari, lakini inatazamiwa kutoa dau katika dirisha kubwa la majira ya joto huku City wakitaka zaidi ya pauni 100 milioni kumruhusu Sane kuondoka.

Hii ni mara ya pili kwa Bayern kurudi kwa Sane baada ya kumsaka kwa nguvu zote katika dirisha kubwa lililopita la majira ya joto kwa ajili ya kuziba mapengo ya wakongwe wao waliotimka klabuni hapo, Arjen Robben na Franck Ribery ambao walitimka klabuni hapo mwishoni mwa msimu uliopita. Sane ameifungia City mabao 25 baada ya kuichezea mechi 89.


Source link

Comments

More in Michezo