Connect with us

Makala

Balinya, Moro warudishwa kikosini Yanga


By Thobias Sebastian

NYOTA wawili wa Yanga, Juma Balinya na Lamine Moro walikosekana katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopita dhidi ya Ndanda ya Mtwara ambapo Yanga ilishinda bao 1-0 katika Uwanja wa Nangwanda Sijaona, Mtwara.
Katika mchezo huo Yanga walianza na wachezaji Farouk Shikhalo, Juma Abdul, Jafary Mohammed, Ally Mtoni, Kelvin Yondani, Kabamba  Tshishimbi, Deus Kaseke, Mapinduzi Balama, David Molinga, Raphael Daud na Patrick Sibomana aliyefunga bao la ushindi.
Katika mchezo huo ambao ulikuwa wa kwanza kwa kaimu kocha mkuu, Boniface Mkwasa aliyechukuwa kwa muda nafasi ya Mwinyi Zahera ambaye siku tatu nyuma kabla ya mchezo huo alitimuliwa.
Katika mchezo wa leo Ijumaa jioni ambao ni wa pili kwa Mkwasa dhidi ya JKT Tanzania huku kikosini Balinya na Moro ambao walikosekana katika mechi na Ndanda wameanza wakichukuwa nafasi za Kelvin  Yondan na Raphael Daud.
Yondani hatacheza mechi hiyo kutokana na kupewa ruhusa ya kupumzika kwani alikuwa kwenye majukumu ya Taifa Stars na Daud.


Source link

Comments

More in Makala