Connect with us

Michezo

Aussems apewe ulinzi mkali – Mwanaspoti


By OLIPA ASSA

KOCHA wa Simba, Patrick Aussems amejikuta anasindikizwa na ulinzi wa polisi zaidi ya wanne baada ya mashabiki kumshangilia na kutaka kumkumbatia.
Kelele za mashabiki zilisikika kwamba “Tunakupenda Uchebe hata kama viongozi hawakutaki, sisi tunakutaka na kukupenda”
Aussems alipewa ulinzi huo mpaka alipoingia kwenye gari la timu bado mashabiki walikuwa wanamchungulia dirishani.
Ukiachana na kocha huyo,  straika Meddie Kagere na Tairone Santos nao walipewa ulinzi mkali baada ya mashabiki kuwavamia ili kupiga nao picha.
Mashabiki wamelalamikia kitendo cha polisi kuwazuia kupiga picha na wachezaji pamoja na kocha wao kwamba hawawatendei haki.


Source link

Comments

More in Michezo