Connect with us

Michezo

Ambokile: Bado nina kazi nzito TP Mazembe


By Olipa Assa

MTANZANIA Eliud Ambokile anayekipiga TP Mazembe amekumbana na changamoto ya kupata namba ndani ya kikosi cha kwanza cha timu hiyo, ingawa amekiri inamjenga kiuwezo.

Tangu ajiunge na timu hiyo msimu huu, Ambokile amesema amecheza mechi moja, amekaa benchi mechi mbili za ligi na moja ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

“Tuliowakuta kwenye mfumo si rahisi kuwatoa kwani na wao hawataki kupoteza namba, hivyo tuna kazi ngumu ya kuhakikisha tunapata namba,”

“Wachezaji wa huku wanaheshimu sana kazi yao, ndio maana soka lao lina ushindani mkubwa, pamoja na kwamba sijafanikiwa kuanza kwenye kikosi cha kwanza ila nimejifunza vitu vingi,”amesema.

Ambokile amesema anaamini akianza kucheza atafanya vitu vikubwa “Hakuna jambo rahisi, soka la huku lipo juu kidogo kuna vitu wametuzidi,”


Source link

Comments

More in Michezo