Je kati ya Neymar na Mbappe nani anayepigiwa upatu kushinda taji la Ballon d’Or

0
17

Je kati ya Neymar na Mbappe nani anayepigiwa upatu kushinda taji la Ballon d’Or

Neymar alipojiunga na Paris St-Germain kwa dau lililovunja rekodi ya £200m msimu uliopita alionekana kuwa mchezaji ambaye atavunja utamaduni wa kushinda taji la Ballon d’Or ambalo Messi na Ronaldo wamekuwa wakishinda.

Lakini wiki nne baadaye kijana nyota Mbappe alijiunga na PSG kwa mkopo kutoka Monaco kabla ya uhamisho huo kuwa wa kudumu baada ya Monaco kulipwa £165.7m.

“Huku Kylian Mbappe na Neymar, wakiwa washambuliaji bora zaidi duniani katika klabu ya PSG ,mwandishi wa gazeti la Le Parisien Yve Leroy aliambia BBC Sport ,” wote wanawania taji la mchezaji bora duniani huku ikijdaiwa kwamba huenda Cristiano Ronaldo na Messi wasishinde”

Huku Neymar aliyekosa siku chache za mwisho za msimu kupitia majeraha, alicheza vyema kushinda Mbappe msimu uliopita katika ligi ya daraja la kwanza ya Ufaransa kwa kila kiwango , lakini huenda mambo yakawa tofauti mwaka huu.

”Mambo yanaweza kubadilika msimu huu , ikitegemea iwapo Neymar atarudia ubora wake” , alisema Leroy.

”Iwapo hilo litafanyika, basi yuko mbele ya Mbappe kwa takwimu na ushawishi”

Walipata uzoefu tofauti katika kombe la dunia.

Huku Neymar akishutumiwa kwa kujiangusha ovyo ovyo kabla ya Brazil kuondolewa katika robo fainali , Mbappe alikuwa kijana wa kwanza kufunga goli katika michuano ya kombe la dunia tangu wakati wa Pele.

Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 19 alifunga mabao manne kwa jumla huku Ufaransa ikishinda kombe hilo, na alichaguliwa na kupewa taji la mchezaji bora wa kombe la Dunia mikongoni mwa vijana.

”Ukitazama muda wa mwisho, basi ni wazi kwamba Mbappe ana fursa. Ameshinda kombe la dunia huku Neymar alipata jeraha na kufanyiwa mzaha kwa hatua yake ya kujiangusha mara kwa mara wakati wa fauli”, alisema Leroy.

Hatahivyo Neymar bado ana umaarufu mkubwa katika klabu ya PSG kwa kuwa ni mchezaji maarufu duniani huku Mbappe akianza kutambulika duniani.

Mbappe anajua kwamba bado hajafikia kiwango cha kusema kwamba yeye ndio bora zaidi na anapendelea kushirikiana na Neymar tu.

Kwa sasa wanaenelewana sana .Itakuwa vyema kumuona Neymar atakavyoshirikiana na Mbappe ambaye anaweza kushinda taji la Ballon d’Or mbele yake

”Neymar hataondoka msimu huu iwapo hakuna kitu cha kushangaza kitakachojitokeza. Swali ni kwamba swali hili litajitokeza tena katika kipindi cha mwaka mmoja ujao”.

”Sina wasiwasi kwamba wanapongezana .wanapenda kutafutana kwa sababu wanacheza safu tofauti. ni Kweli kwamba mbinu hizi zote lazima zithibitishwe uwanjani”.

Mbappe ni miongoni mwa wachezaji watatu wanaopigiwa upatu kushinda taji hilo la Ballon d’Or ikilinganishwa na Messi.

Huu unaweza kuwa mwaka wa kwanza tangu 2010 kwamba Messi na Ronaldo waliopigiwa upatu kushinda taji hilo siku za nyuma kutoshinda taji hilo.

Raia wa Croatia na kiungo wa kati wa Barcelona Luka Modric ni wa pili huku Neymar akiwa wa tatu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here