Cheikhou Kouyate: Crystal Palace wamsajili mchezaji wa West Ham

0
16


Cheikhou KouyateHaki miliki ya pichaREUTERSImage captionCheikhou Kouyate aliichezea Senegal mara tatu katika Kombe la Dunia Urusi

Crystal Palace imemsajili mchezaji wa kiungo cha kati Cheikhou Kouyate kutoka West Ham katika mktaba wa miaka minne kwa kitita kisichojulikana.
Raia huyo wa Senegal mwenye umri wa miaka 28 alikaa kwa misimu minne na West Ham na kuwahi kushiriki mechi 129 na kufunga magoli 12.
Anakuwa mchezaji wa pili wa timu ya taifa hiyo ya Mwewe kusajiliwa msimu huu wa joto baada ya kipa Vicente Guaita kuwasili kutoka Getafe.

data

“Huu ndio wakati muafaka kuhama kwasababu nilihitaji changamotompya,” Kouyate ameiambia runinga ya Palace.
“NIna kumbukumbu nzuri za West Ham lakini ninahitaji kuja hapa na kuonyesha uweledi wangu kwasababu napenda mpango huu wa Crystal Palace.”

Cheikhou KouyateHaki miliki ya pichaREUTERS

by richardshiyo@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here