Yanga kumtambulisha wawa ijumaa

0
7

Beki wa ivory coast Pascal Wawa (pichani)
UONGOZI wa Yanga unaendelea kufanya usajili kimyakimya na umakini mkubwa kwa ajili ya kuimarisha kikosi chao ambapo wamepanga kuwatambulisha wache­zaji wote waliowasajili ijumaa ijayo.
Yanga wamesema kuwa watawatambulisha wache­zaji hao siku hiyo kwa kuwa ndiyo usajili utakuwa ume­funguliwa.
Timu hiyo hivi karibuni ilitangaza kufanya usajili wa kimyakimya kwa hofu ya wapinzani Simba na Azam FC na Azam FC kuwazidi ujanja na kuwasajili kama ili­vyokuwa kwa Adam Salam­ba, Habib Kiyombo, Marcel Boniventure na Mohamed Rashid waliokuwa wanawa­wania Yanga.
Yanga hadi sasa tayari imefanikiwa kumbakisha beki wao mkongwe, Kelvin Yondani aliyekuwa ana­waniwa na Simba, huku ikielezwa kumsajili msham­buliaji mpya Mbenin, Marcelin Degnon Koupko na beki raia wa Ivory Coast, Pascal Wawa.
Akizungumza na Cham­pioni Ijumaa, Katibu Mkuu wa Yanga, Boniface Mkwasa alisema tayari imemalizana na baadhi ya wachezaji kwa kusaini mikataba ambao majina ni siri.
“Klabu zinavyofanya usajili kwa hivi sasa zinakiuka kanuni kwa kuwa dirisha la usajili bado halijafunguliwa.
“Lipo wazi hilo, klabu zi­nazosajili hivi sasa zinaen­da kinyume na utaratibu wa usajili na hiyo ni kutokana na dirisha la usajili kutofunguliwa.
“Sisi kama Yanga tumepanga kuwatambulisha usajili wa wachezaji wetu wapya baada ya dirisha la usajili kufunguliwa na tu­mepanga kufanya usajili kutokana na map­endekezo ya kocha ambayo ameyatoa kwa uongozi.
“Mashabiki na Wanacha­ma wetu wa Yanga wavute subira, muda ukifika kila kitu tutakiweka wazi kwa maana ya kutangaza usajili wa wachezaji tuliowasajili,” alisema Mkwasa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here