Wanachama wa Yanga Waandamana Hadi Nyumbani kwa Manji Kumuomba Arudi Kwenye Nafasi Yake

0
19

Katika hali isiyo ya kawaida inaelezwa baadhi ya mashabiki na wanachama wa Yanga wameendeleza kauli mbiu ya Mabadiliko na Yanga kwa kuamua kutimba nyumbani kwa tajiri Yusuf Manji kufikisha kilio cha kumtaka abadilishe maamuzi ya kutaka kujiuzulu nafasi yake.


Mapema tu baada ya Mkutano Mkuu wa Klabu ulifanyika Juni 10 kwenye Ukumbi wa Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oyster Bay, walikusanyika na daladala mbili kwenda moja kwa moja katika makazi ya Manji.


Mara baada ya kuwasili taarifa zinaeleza hawakufanikiwa kumkuta na badala yake walikutana na mlinzi aliyewaambia kuwa bosi wake hayupo akieleza amesafiri. Wanachama hao ilibidi wamwachie ujumbe mlinzi huyo wakiomuomba amwambie kuwa bado anahitajika katika kiti cha Uenyekiti ndani ya klabu.


Hatua hiyo imekuja mara baada ya Manji aliyetarajiwa kufika kwenye mkutano huo kushindwa kuwasili na kuleta sintofahamu kama anaweza akarejea kwenye nafasi yake.


Ikumbukwe Maji alijiuzulu nafasi ya Uenyekiti Mkuu Yanga kwa maelezo ya kuwa alikuwa anahitaji kupumzika na badala yake nafasi yake ikawa chini ya Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ligi ya TFF.


Katika Mkutano Mkuu uliofanyika Juni 10 jumla ya wanachama 1,400 waliohudhuria walipinga barua ya Manji iliyosema amejiuzulu na kuazimia moja kwa moja kuwa ataendelea kusalia kama Mwenyekiti wao. 

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here