Ujerumani watuma salamu za vitisho kuelekea kombe la dunia nchini Urusi

0
11


Mabingwa
watetezi wa Kombe la Dunia, Ujerumani jana usiku wameitwanga timu ya
taifa ya Saudi Arabia goli 2-1 kwenye mchezo wa kirafiki kuelekea
michuano ya kombe la dunia inayoanza kutimua vumbi alhamisi ijayo.

Magoli ya Ujerumani yamefungwa na Timo Werner na Omar Hawsawi
aliyejifunga mwenyewe huku Saudia goli lao likifungwa na Taisir
Al-Jassim.

Kwenye mchezo huo, Nahodha Manuel Peter Neuer alitolewa na kuingizwa
kipa wa Barcelona, Marc-André ter Stegen dakika chache baadae baada
kuingia aliokoa mkwaju wa penati.

Kwenye mchezo huo ambao Ujerumani ilionekana kuutawala mpira katika
vipindi vyote viwili inaonesha picha kuwa huenda mwaka huu wakanyanyua
tena kombe la dunia.

by richard@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here