Ufisadi: Refa Mkenya aliyeteuliwa na Fifa Kusimamia kombe la dunia ‘anaswa’

0
6

Mwandishi wa habari wa Ghana Anas Aremayew Anas akihojiwa na wanahabari kuhusu makala yake ya upelelezi yaliochukua miaka miwilitakriban maafisa 100 wa kandanda
katika eneo la Afrika Magharibi na Kenya walipatikana katika kamera
wakipokea fedha katika operesheni kali.
Ni miongoni mwa upelelezi
wa miaka miwili uliofanywa na mwandishi wa Ghana mwenye utata Anas
Aremeyaw Anas. Kipindi cha BBC Africa Eye kimepata kanda za video za
kipekee katika makala yao ya mwisho.
Katika kisa kimoja naibu refa
kutoka Kenya anayeelekea Urusi kuchezesha dimba la dunia kutoka Kenya
alikubali dola 600 kutoka kwa mtu aliyejifanya kuwa afisa wa shirikisho
la soka la Ghana.
Fifa inasema kuwa refa huyo kwa Jina Aden Range Marwa , ambaye
ni mmojawapo wa marefa walioteuliwa na Fifa kushiriki katika kombe la
dunia nchini Urusi , hataelekea tena Urusi baada ya kupatikana akipokea
zawadi ya $600.
Marwa alipewa fedha hizo na mwandishi mpelelezi
aliyejifanya kuwa afisa mkuu wa timu moja kuu ya Ghana. Hatahivyo refa
huyo amekana kufanya makosa yoyote.
Mwanachama wa baraza la Fifa
nchini Ghana Kwesi Nyantakyi , ambaye ndiye afisa wa pili kwa uwezo
katika soka ya Afrika , pia alipatikana na operesheni hiyo kali.
Alionekana akipokea $65,000 kutoka kwa mwandishi mpelelezi aliyejifanya kuwa mwekezaji katika soka ya Ghana.
Nyantakyi
amekataa kutoa tamko lolote. Kwa jumla zaidi ya marefa 100 na maafisa
wakuu walipatikana katika kamera wakichukua fedha kinyume na sheria za
Fifa na GFA .
Makala hiyo iliofanywa na mwandishi aliyezua utata
Anas Aremayaw Anas imezua maswali makali kuhusu hatma ya mchezo wa
kandanda wenye ushabiki mkubwa barani Afrika.

by richard@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here