Tetesi za soka Ulaya Jumanne 05.06.2018

0
1
ZidaneMshambuliaji wa Liverpool na Senegal
Sadio Mane, 26, alikubali kujiunga na Real Madrid kabla ya Zinedine
Zidane kujiuzulu kama kocha wa mabingwa hao wa Ulaya. (France Football –
in French)

Matumaini ya Chelsea ya kumzuia Eden Hazard yamepigwa
jeki na hatua ya Zidane kuondoka Real. Raia huyo wa Ufaransa aliambia
mabingwa hao wa Uhispania kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27
msimu ujao. (London Evening Standard)

Felipe Anderson, 25

Zidane alijiuzulu katika Real Madrid kutokana na
mipango ya dirisha la uhamisho la msimu ujao. Klabu hiyo ilikuwa ikitaka
kumnunua Kipa wa Manchester United na Uhispania David De Gea 27, lakini
Zidane hakutaka. Pia alikasirika kwamba mpango wake wa kutaka kumsajili
Hazard haikuungwa mkono. (Sun)
Leicester imefufua hamu yake ya kumsajili mshambuliaji wa
Manchester City na raia wa Uingereza Patrick Roberts, 21, ikiwa ni
miongoni mwa dau la £60m ambalo litahakikisha kuwa winga wa Algeria
Riyad Mahrez, 27, anajiunga na viongozi hao wa ligi. (Daily Telegraph)

Mkufunzi wa Tottenham Mauricio Pochettino alikataa
kuwa mkufunzi wa Real Madrid kwasababu hakutaka kuonekana kuwa anapenda
fedha zaidi. (Daily Mail)
Arsenal inapanga uhamisho wa Marouane
Fellaini, 30, ambaye kandarasi yake katika klabu ya Manchester United
inakamilika mwezi huu. (Daily Mirror)
Beki
wa kulia wa Ureno Diogo Dalot, 19, atafanyiwa uaguzi wa matibabu wiki
hii kabla ya kujiunga na klabu hiyo kutoka Porto..(Sky Sports)

Sokratis Papastathopoulos anatarajiwa kujiunga na
Arsenal kwa dau la £16m kutoka Borussia Dortmund – baada ya beki huyo wa
Ugiriki mwenye umri wa miaka 29 kukataa kujiunga na Manchester United,
kulingana na babake. (Radio 24/7 via Daily Mirror)
Tottenham
haiko katika mazungumzo na Manchester United kuhusu uuzaji wa beki Toby
Alderweireld, licha ya madai yanayomuhusisha mchezaji huyo wa Ubelgiji
29 na uhamisho wa kuelekea Old Trafford. (Football.London)

Klabu ya Crystal Palace iko tayari kumuuza Christian Benteke

Ombi la West Ham la 38m kumnunua kiungo wa kati wa
Lazio na Brazil Felipe Anderson, 25, limekataliwa (Gazzetta dello
Sport, via Daily Express)
Klabu ya Crystal Palace iko tayari
kumuuza Christian Benteke msimu ujao huku hatma ya mchezaji huyo ikiwa
haijulikani baada ya kuwachwa nje katika kikosi cha kombe la
dunia(London Evening Standard)

Leroy Sane aliyewachwa nje ya kikosi cha Ujerumani

Leicester inapanga kumnunua mshambuliaji wa klabu ya Uturuki ya Trabzonspor’s Abdulkadir Omur 18. (Leicester Mercury)
Newcastle
inataka kumuuza mchezaji wa Senegal Henri Saivet, 27, msimu huu ,
lakini hamu ya mchezaji huyo ni kuendelea kucheza kwa mkopo (Newcastle
Chronicle)
Kinda wa Tottenham Reo Griffiths anatarajiwa kusalia
katika klabu hiyo msimu huu. Mchezaji huyo wenye umri wa miaka 17
aliifungia klabu hiyo yenye wachezaji wasiozidi umri wa miaka 18 magoli
30 na alikuwa anapangiwa kuelekea Bundesliga. (London Evening Standard)

Mkufunzi wa West Brom Darren Moore anataka kumzuia
James Morrison, ambaye kandarasi yake inakamilika mwisho wa msimu huu
iwapo kiungo huyo wa kati mwenye umri wa miaka 32 raia wa Uskochi
ataonyesha kiwango kizuri cha mchezo wake. (Express and Star)
Bango
kubwa la winga wa Manchester City Leroy Sane liliangushwa baada ya
nyota huyo mwenye umri wa miaka 22 kuwachwa nje katika kikosi cha kombe
la dunia cha Ujerumani. (Daily Mail)
Mmiliki wa Liverpool John W
Henry anasema kuwa klabu za ligi ya Uingereza zinafaa kulipwa kitita
kikubwa cha mapato ya runinga ughaibuni. (Times)

by richard@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here