Tetesi za soka Ulaya 01.06.2018

0
10
Kocha wa Real Madrid anayeondoka Zinedine Zidane na Mshambuliaji Gareth BaleChelsea itajaribu kumshawishi Zidane kuwa mkufunzi wake mpya . (sun)

Matumaini
ya klabu ya Manchester United ya kumsajili Gareth Bale, 28, huenda
yakafifia huku mchezaji huyo wa taifa la Wales akitarajiwa kusalia
kufuatia kuondoka kwa Zidane. (Daily Mirror)

Real Madrid huenda ikamnyatia mkufunzi wa Tottenham
Mauricio Pochettino – ambaye alitia saini mkataba mpya wa miaka mitano
na timu yake wiki iliopita- ili kuchukua mahala pake Zinedine Zidane
aliyeondoka. (Daily Mirror)
Lakini Real pia inamtaka kocha wa
Liverpool Jurgen Klopp, amaye aliiongoza The Reds kufika fainali ya
kombe la vilabu bingwa Ulaya. (Sun)
Kandarasi ya Pochettino katika klabu ya Spurs haina kipengee
ambacho kinaweza kumruhusu kuondoka na mwenyekiti wake Daniel Levy yuko
tayari kuhakikisha kuwa anasalia katika klabu hiyo.(Daily Telegraph)

Napoli Maurizio Sarri

The Blues pia huenda wakamlenga mkufunzi wa Ufaransa
na Paris St-Germain Laurent Blanc kuchukua mahala pake Antonio Conte.
(Daily Mail)
Chelsea inasema kuwa haitalipa dau la £7m ili kununua kandarasi ya mkufunzi wa Napoli Maurizio Sarri. (Guardian)

Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich

Mmiliki wa Chelsea Roman Abramovich angependelea kulipwa kitita cha £1.17bn iwapo ataamua kuiuza Chelsea (Times)
Chelsea
imesitisha mazungumzo ya kandarasi mpya na kipa wake Thibaut Courtois
na huenda wakamuuza raia huo wa Ubelgiji mwenye umri wa miaka 26. The
Blues inalenga kumsajili kipa wa Roma na Brazil Alisson, 25. (Sky
Sports)

Gonzalo Higuain

Juventus imeiuliza Chelsea iwapo inamhitaji
mshambuliaji wa Argentina Gonzalo Higuain, 30, ikiwa ni katika mipango
ya kumsajili tena mshambuliaji wa Uhispania Alvaro Morata, 25. (London
Evening Standard)
Kocha mpya wa Arsenal Unai Emery anataka kumnunua kiungo wa kati kinda Yacine Adli 17 kutoka Paris St-Germain.

Unai Emery

Mchezaji huyo anayeichezea timu ya taifa ya Ufaransa
ya wachezaji wasiozidi umri wa miaka 18 pia amevutia timu kama vile
Bayern Munich, Barcelona na Real Madrid. (London Evening Standard)
Newcastle
imehusishwa na beki wa klabu ya Sassuolo 26 Gian Marco Ferrari, ambaye
alihudumu msimu uliopita kwa mkopo katika klabu ya Sampdoria.
(Newcastle Chronicle)

Peter Schmeichel, 54

Kipa wa zamani wa Manchester United Peter
Schmeichel, 54, anakaribia kujiunga na klabu ya Sporting kama mkufunzi
wa kipa. (Correio da Manha, via Sport Witness)
Aliyekuwa mkufunzi
wa klabu ya Spurs Harry Redknapp anaamini kwamba mpwa wake , Frank
Lampard, anafaa kumsajili nahodha wa zamani wa Chelsea Jhn Terry, 37,
katika klabu ya Derby. (Talksport)

Harry Redknapp

Manchester United inatafuta kumsajili afisa wa
kusaka wachezaji nchini Ufaransa huku Klabu hiyo ikiendelea kuimarisha
mtandao wake wa utafutaji wa wachezaji wenye vipawa . (Manchester
Evening News)

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here