Niyonzima nje simba akicheza fainali kesho dhidi ya gor mahia

0
11

-Kiungo fundi wa Klabu ya Simba Sc, Haruna Niyonzima kesho atakosekana kwenye mchezo wa fainali ya michuano ya Sportpesa Super Cup dhidi ya Gor Mahia ya Kenya kutokana kuwa na kadi mbili za njano.

-Sheria ya Michuano ya Sportpesa Mchezaji akipata kadi mbili za njano anapaswa kukosa mchezo unaofuata (mchezo wa tatu) Niyonzima alipata kadi kwenye mchezo wa robo fainali dhidi ya Kariobangi Sharks na ule wa nusu Fainali dhidi ya Kakamega Home Boyz.

-Kukosekana kwa Niyonzima klabu ya Simba imebaki na wachezaji 17 tu ambao watacheza fainali kesho ambao ni magolikipa Aishi Manula na Ally Salim mabeki ni Ally Shomary, Shomary Kapombe, Mohamed Hussen, Yusuph Mlipili, Erasto Nyoni na Paul Bukaba.

-Viungo wapo Jonas Mkude, Mzamiru Yassin, Mohamed Ibrahim, Rashid Juma na Shiza Kichuya safu ya ushambuliaji wapo Mohamed Rashid, Moses Kitandu, Marcel Kaheza na Adam Salamba

-Pia wachezaji wawili Emmanuel Okwi na Asante Kwasi ambao kocha Masoud Djuma aliwahitaji kwa ajili ya kukiongezea nguvu kikosi hicho kwenye mchezo wa fainali mpaka sasa hawajaripoti Kenya.

-Uongozi wa klabu hiyo umesema wachezaji walipo Kenya ndio watacheza mchezo wa fainali dhidi ya Gor Mahia hawatarajii kuongeza mchezaji yoyote.
@yossima Sitta Jr.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here