Mwambusi arejea kama kocha msaidizi wa hans pluijm azam

0
6

Kocha Juma Mwambusi amerejea tena katika soka na kujiunga na klabu ya Azam FC.

Mwambusi amesaini mkataba wa miaka miwili na anaungana na Kocha Hans van der Pluijm raia wa Uholanzi ambaye kabla alizinoa Yanga na Singida United.

Mara ya mwisho Mwambusi alikuwa Yanga ambayo alikuwa msaidizi wa Kocha George Lwandamina.

Kabla ya kuwa chini ya Lwandamina raia wa Zambia, Mwambusi alifanya kazi kwa mafanikio chini ya Pluijm wakiwa Yanga.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here