Morocco achukua mikoba Pluijm

0
4
Singida United imemtambulisha kocha, Hemed Morocco kuchukua mikoba ya Mholanzi Hans Pluijm ‘Babu’ aliyetimkia Azam FC.
Morocco ni kocha msaidizi wa timu ya Taifa Stars ametangazwa kuchukua majukumu hayo baada ya mechi ya fainali ya FA kati ya Singida United na Mtibwa Sugar.
 Uongozi wa Singida haukuweka wazi muda wa mkataba ambao Morocco amesaini, lakini wamesisitiza kumpa ushirikiano ili timu hiyo iwe na mafanikio.
Meneja wa Singida United, Festo Sanga amesema: “Morocco ndiye atakayekuwa kocha wetu mkuu na kikubwa tunamuahidi kumpa ushirikiano wote.”
Naye Morocco alisema: “Nashukuru kuwepo hapa, nafikiri Singida wameangalia vigezo vingi ndiyo maana wakaamua kunichukua,  naahidi kuwa nitaifanya kazi kubwa, kikubwa ni ushirikiano.”
Katika kuandaa kikosi chake ili kiende na mfumo anaouhitaji, Morocco amesema, atatumia nafasi ya Kenya ambapo wanaenda kushiriki mashindano ya SportPesa ili kupata timu anayoihitaji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here