Liverpool wakaribia kumnunua mchezaji mwingine nyota kutoka Ufaransa.

0
8
Liverpool wanakaribia kumnunua mchezaji mshambuliaji nyota wa Ufaransa Nabil Fekir.
Mazungumzo kati ya klabu ya Liverpool na Lyon yanatarajiwa kukamilika Ijumaa kuhusu uhamisho ambao huenda ukawa wa thamani ya karibu euro 60m (£52.75m) – 55m (£48.35m) na malipo ya ziada ya karibu euro 5m (£4.4m) add-ons.
Hata hivyo, Lyon wamekataa “kata kata” kwamba mchezaji huyo anakaribia kuhama, kwenye ujumbe waliouandika kwenye Twitter Ijumaa.
Nahodha huyo wa Lyon mwenye miaka 24 ni miongoni mwa wachezaji wanaotafutwa sana na meneja wa Liverpool Jurgen Klopp kipindi cha sasa cha kuhama kwa wachezaji.
Mwenyewe inadaiwa anataka sana kuhamia Anfield.
Fekir anatarajiwa kusafiri na kikosi cha Ufaransa kwenda kucheza Kombe la Dunia Urusi, ambapo mechi yao ya kwanza itakuwa dhidi ya Marekani Jumamosi.
Rais wa Lyon Jean-Michel Aulas anafahamika kwa kuwa mkali sana kwenye mazungumzo kuhusu uhamisho wa wachezaji. Ijumaa ni siku muhimu sana kwa mazungumzo kuhusu mchezaji huyo kwani Liverpool wanaonekana kutaka sana kukamilisha mkataba huo kabla ya wikendi.
Kuwasili kwa Fekir huenda kukawa ishara ya karibuni ya azma ya Liverpool, waliofika fainali Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya lakini wakashindwa na Real Madrid, ya kujiimarisha zaidi tayari kwa msimu ujao.

Fabinho na Naby Keita

Tayari wametoa £39m kumnunua kiungo wa kati wa Brazil Fabinho kutoka Monaco.
Naby Keita naye anatarajiwa kujiunga na kutoka RB Leipzig ya Ujerumani Julai kwa uhamisho wa £52.75m.
Liverpool pia wanatafakari uwezekano wa kutumia kifungu cha £12m kwenye mkataba wa Xherdan Shaqiri kumfungua kutoka kwenye klabu ya Stoke City baada yao kushushwa daraja hadi ligi ya Championship.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here