Kyombo atua Singida United

0
7
Dar es Salaam: Mshambuliaji aliyezitesa Simba na Yanga katika Ligi Kuu Bara msimu huu, Habib Kyombo amejiunga na Singida United leo.
Mshambuliaji huyo wa Mbao, Kyombo amekuwa mfungaji bora wa mashindano Kombe la Shirikisho  baada ya kufunga mabao sita, ametamburishwa rasmi kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha baada ya mchezo wa fainali wa FA kati ya Singida United na Mtibwa Sugar.
Singida ilishawishika kumsajili Kyombo baada ya kufanya vizuri katika Ligi Kuu na mashindano ya FA ambapo aliifunga  Yanga mabao mawili peke yake, Mbao ikashinda 2-0, kwenye Uwanja wa CCM Kirumba.
Pia aliifunga Simba bao moja, Mbao ikamaliza kwa sare ya mabao 2-2. Pia Kyombo amemaliza Ligi Kuu akiwa amefunga mabao tisa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here