Kumbe kisa mkataba kocha simba lechantre asusa

0
10

-Makocha wa Simba kocha mkuu wa klabu ya Simba Sc, Pierre Lechantre na kocha wa viungo Aimen Habib wamesusa klabu hiyo kwa sababu ya kutopewa mkataba mpya.

-Katika Mchezo wa leo wa nusu fainali dhidi ya Kakamega Home Boyz makocha hao wamekaa jukwaa na timu kuongozwa na kocha msaidizi wa klabu hiyo Masoud Djuma.

-Kocha mkuu wa klabu ya Simba Sc, Pierre Lechantre amekasilishwa na viongozi wa klabu hiyo kumchunia kumpa mkataba mpya na amekuwa akisakamwa kila kukicha na baadhi ya viongozi na mashabiki wa klabu ya Simba.

-Pierre Lechantre ambaye alisaini mkataba wa miezi 6 january 19 na utaisha June 19 mwezi huu Kutokana na hali hiyo kocha huyo amegoma kuendelea kuwa kocha wa klabu hiyo mpaka ajue hatma yake ndani ya klabu hiyo.

-Pia habari za ndani kutoka ndani ya klabu ya Simba zinadai kocha huyo amekuwa hana amelewano mazuri kocha msaidizi wa klabu hiyo Masoud Djuma ndio maana viongozi wamegoma kumpa mkataba mpya na wanasubili mkataba wake uishe ili aondoke.

-Pia imebainika kuwa Kocha Pierre Lechantre hakutaka Masoud Kuwa kocha msaidizi wa klabu hiyo na alikuja na Aimen Habib awe kocha msaidizi wa klabu hiyo ila Simba walimgomea kwa sababu Masoud Djuma alikuwa tayari na mkataba.

-Kocha Lechantre alikuwa anamjua Aimen Habib kama msaidizi wake namba moja huku Masoud Djuma akimtambua kama kocha msaidizi namba mbili wakati Simba wanamtambua Masoud Djuma kama kocha msaidizi na Habib kama kocha wa viungo.

-Viongozi wa klabu ya Simba Sc wamegoma kuzungumzia kususa kwa kocha huyo huku wakisema watalitolea ufafanuzi baada ya kumalizika kwa michuano ya Sportpesa Super Cup.
@yossima Sitta Jr.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here