Kombe la dunia na vibweka tarajiwa

0
9
BangladeshMkulima mmoja mwenye asili ya
Bangladeshi ameonesha uungaji mkono wa aina yake kwa timu ya Ujerumani
inayoshiriki kombe la dunia kwa namna ambayo si ya kawaida, baada ya
kutengeneza bendera yenye urefu wa kilomita 5.5 ama maili 3.4.

Mkulima
huyo anaitwa Amjad Hossain, mwenye umri wa miaka 69, ameelezea mapenzi
yake kwa nchi ya Ujerumani baada ya kutumia dawa kutoka nchini humo
kutibu tatizo la homeopathic.
Amjad alianza zoezi la utengenezaji
bendera hiyo miaka miwili baadaye, baada ya ujerumani kuwa mwenyeji wa
michuano ya kombe la dunia mnamo mwaka 2016, na imeendelea kuongezea
katika mashindano yaliyo fuata.Hosain alidiriki kuuza hata ardhi
aliyokuwa anaimiliki ili mradi tu anunue kitambaa cha kutosha,chenye
rangi nyeusi, nyekundu na dhahabu.

Bangladesh

Bendera hiyo ilizinduliwa rasmi mapema wiki hii
katika shule ambayo bwana Hossain kwenye mji alikozaliwa wa Magura, kama
maili 60 sawa na kilomita mia moja upande wa kuelekea magharibi mwa mji
mkuu Dhaka.
Kwa muujibu wa shirika la habari la AFP, Amjad
anapanga kuionesha bendera hiyo katika viwanja vya kwao ikiwa Ujerumani
itainfia nafasi ya pili katika michuano hiyo ya kombe la dunia na kusema
kuwa anamapenzi ya dhati kwa timu hiyo.Amenukuliwa akisema analipenda
soka la Ujerumani , wanatandaza kandanda murua .
Wakati wa
michuano ya kombe la dunia la mwaka 2014, wakati bendera yake ilipokuwa
na urefu wa kilomita 3.5 tu – balozi wa Ujerumani nchini Bangladeshi
alimpa Amjad uanachama rasmi na wa maisha wa klabu ya taifa la
Ujerumani na shabiki wa kudumu wa timu hiyo , akapewa pia mpira, jezi ya
timu hiyo pamoja na cheti cha utambuzi.
by richard@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here