Kipa wa Tunisia ‘asingizia jereha’ swali kwanini??kufungua mwezi wa Ramadhan

0
10
Kipa wa Tunisia Mouez Hassen alala uwanjani

Kikosi cha kombe la dunia cha
Tunisia kimepata njia ya kukabiliana na uchovu huku wakiendelea kufunga
mwezi mtukufu wa Ramadhan.

Katika mechi za kirafiki dhidi ya
Ureno , aliyekuwa kipa wa Uturuki, Mouez Hassen alionekana kusingizia
jeraha wakati funga hiyo ilipokamilika saa za jioni.
Alipokuwa akilala uwanjani ili kupata matibabu , wachezaji wenzake walikimbia hadi nje ya uwanja ili kunywa maji na tende.
Na hatua hiyo ilileta matokeo. Wakiwa nyuma 2-1 dhidi ya mabingwa wa
Ulaya 2-1 Ureno, Tunisia walisawazisha dakika sita baada ya jeraha la
Hassen na hivyobasi kumaliza mechi hiyo ikiwa 2-2.
Siku chache baadaye dhidi ya Uturuki, Hassen alisitisha mchezo kwa kulalia mgongo wake.
Kwa
mara nyengine wachezaji wenzake walikula tende na kunywa maji
waliyopewa na wahudumu wa kitendo cha ukufunzi . Mechi hiyo ilikwisha
2-2.
Ali Maaloul anakula tende
Wachanganuzi nchini Tunisia kwa haraka walichunguza wakati kipa huyo
aliposingizia kuumia katika mechi zote mbili katika dakika ya 58 na 47
mtawalia.
Muda huo uliingiana na muda wa Iftar ambapo Waislamu
hufungua mwezi wa Ramadhan kwa kula tende na maji. Shirikisho la soka
nchini Tunisia bado halijazungumzia kuhusu mapumziko hayo ya jeraha.
Lakini
kipa Hassan alituma ujumbe wa Twitter: ”Niliumizwa, [akiweka emoji za
kucheka]’ akimjibu mchezaji mwenza Chaker Alhadhurt aliyejibu: ”Ni sawa
sasa tunajua ulikuwa aukidanganya”

by richard@spoti.co.tz

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here